29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Kizimbani kwa kuomba rushwa ya milioni 50

BEATRICE KAIZA

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Mkoa wa Ilala, inamshikilia Katibu Mkuu wa Chama cha kijamii (CCK), Renatus Muabhi kwa kosa la kujifanya mtumishi wa Serikali kutoka katika taasisi hiyo na kuomba rushwa ya kiasi cha Sh 50,000,000.

Akizungumza na Mtanzania Digital Mkurugenzi wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amesema uchunguzi wa takukuru umebaini kuwa dhumuni lake lilikuwa  ni kuomba rushwa hiyo ili kumsaidia Mkurugenzi wa kampuni ya Bharya Engeneering & Contracting Company Limited (BECCO), Manraj Bharya katika tuhuma zake zilizokuwa zikimkabili.

“Mtuhumiwa alikamatwa Desemba 12 mwaka huu katika ofisi za kampuni ya BECCO akiwa amepokea fedha za mtego wa rushwa kiasi cha Sh. 1,000,000,’’ amesema Myava.

Pia Myava ametoa rai kwa wananchi kujihadhari na matapeli wa aina hiyo na kujiepusha nao, na endapo wakibaini wahalifu wowote watoe taarifa Takukuru ili uchunguzi ufanyike ili waweze kubainika na kuchuliwa hatua stahiki.

Uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles