POLISI WAMCHUNGUZA MO SALAH

0
401

Merseyside, Uingereza


Mshambuliaji wa Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah anachunguzwa na polisi baada ya kuonekana kwenye video akiendesha gari huku akitumia simu.

Habari za ndani za taarifa hizo zinaeleza kwamba polisi wamepewa taarifa za mshambuliaji huyo na viongozi wa klabu hiyo.

Hata hivyo msemaji wa Liverpool amesema waliwafahamisha polisi kuhusu video hiyo baada ya kuzungumza na mchezaji huyo.

“Tumezungumza na mchezaji huyo na tutashughulikia hatua nyingine zozote zinazohitajika kuchukuliwa kwa kutumia mifumo ya ndani. Hakuna taarifa nyingine kuhusu tukio hili itakayotolewa na klabu wala mchezaji mwenyewe,” alisema msemaji huyo.

Polisi wa Merseyside wamethibitisha kupitia ukurasa wao wa Twitter na kudai kwamba video hiyo imekabidhiwa idara husika kwa utekelezaji.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here