24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

KENYA, SUDAN, DJBOUT NA ETHIOPIA KUKIPIGA LEO U17

NALULU RINGO


Mashindano ya vijana chini ya miaka 17 kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yanaendelea leo katika Uwanja wa Chamanzi jijini Dar es salaam ambapo Kenya itamenyana na South Sudan, Dijbout na Ethiopia.

Katika mashindano hayo jana Rwanda iliinyuka Burundi kwa mabao 4-3. Mwenyeji wa mashindano hayo Tanzania atacheza siku ya Alhamis kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya Rwanda, huku Somalia akicheza na Burundi Uwanaja wa Chamazi.

Mashindano hayo yapo kundi A na kundi B yenye jumla ya timu 9 kundi A lina timu 4 na Kundi B lina timu5.

Kundi A linaongozwa na Rwanda yenye alama 6 akiwa ameshacheza michezo miwili ikifuatiwa na Tanzania yenye alama 3 ikiwa imeshacheza mchezo 1 huku Somalia na Burundi wakilingana kwa kutokuwa na alama.

Kundi B linaongozwa na Ethiopia mwenye alama tatu akiwa amecheza mchezo mmoja ikifuatiwa na Sudan yenye alama tatu mchezo mmoja huku Djbouti na Kenya wakifanana kwa kutokuwa na alama.

Ikumbukwe kuwa bingwa wa mashindano hayo atapata fursa ya kushiriki mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana chini ya miaka 17 Afrika yaliyoandaliwa na CUF ambayo amepangwa kufanyika mwakani nchini Tanzania ambapo kama mwenyeji ataibuka na kombe mshindi wa pili atapata nafasi ya upendeleo itakayotolewa na mshindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles