24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Papa ‘hutibu’ saratani, uzee

FROLIDA, MAREKANI

PAPA aina ya ‘great white’ inawezekana wakawa wanashikilia siri za kutibu saratani na maradhi mengine yanayoambatana za uzee.

Watafiti kwa kutumia mfumo wa vinasaba wa papa hao wamebaini pingili ambazo zinawalinda samaki hao dhidi ya saratani na magonjwa mengine. Wanasayansi wanaamini utafiti zaidi unaweza kusaidia kutimia matokeo hayo katika kutibu magonjwa yatokanayo na umri mkubwa kwa binadamu.

Aina hiyo ya papa wanaweza kujitibu vinasaba vyao katika namna ambayo haiwezekani kwa vinasaba vya binadamu. Utafiti huo umefanyika katika Chuo Kikuu cha Nova Southeastern Florida cha nchini hapa.

Jeni, au sehemu ya vinasaba inayorithisha tabia au maumbile fulani, ambazo si thabiti za binadamu ndizo zinazosababisha watu kupata maradhi ya saratani na mengine ambayo huendana na uzee.

Vinasaba vya papa ni vikubwa kwa mara moja unusu zaidi ya binadamu, hiyo ina maana kuwa kuna vitu samaki hao wanaweza kuvifanya ambayo binadamu hawawezi.

Na wanasayansi sasa wanatazamia kufumua siri hizo ili kutatua maradhi hayo kwa binadamu. Pia papa hao wanatazamiwa kusaidia matibabu ya kuzuia damu kuvuja sababu wana uwezo mkubwa wa kupona majeraha hatari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles