Mwanamke mmoja nchini Vietnam amekiri kutoa mguu na sehemu ya mkono wake vikatwe ili aweze kudai malipo ya bima, kwa mujibu wa polisi.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 , anayetambuliwa kama ”Ly Thi N”, alidanganya kuwa aligongwa na treni, limeripoti gazeti la polisi nchini Vietnam.
Lakini kwa sasa ameripotiwa kukiri kwamba alimlipa rafiki yake dola $2,200 akate viungo vyake.
Lengo lilikua ni kudai dola zaidi ya $150,000 kutoka kwa kampuni ya bima yake.
Kwasasa mwanamke huyo akiwa amepona majeraha yake. anaendesha biashara kwa shida, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.
Â