24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kondakta kortini kwa kutishia kumuua Rais Magufuli

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

KONDAKTA wa daladala, Hamimu Seif (42)   amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kutishia kumuua kwa maneno, Rais Dk. John Magufuli.

Mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa  mtaa wa Ujiji, Mwananyamala, alipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa na kusomewa shtaka na wakili wa serikali Mwandamizi, Kenneth Sekwao.

Sekwao alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya Soweto iliyopo   Makumbusho,Wilaya ya Kinondoni,Dar es Salaam.

Ilidaiwa   kwamba mshitakiwa alitishia kumuua Rais Magufuli kwa kutamka  maneno kuwa, ‘Kwa mambo anayoyafanya Rais Magufuli, nipo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza’.

Mshtakiwa   alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulisema upelelezi haujakamilika.

Hakimu Riwa alikubali kumpa dhamana mshtakiwa kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni mbili.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na alirudishwa rumande hadi Aprili 21 mwaka huu kesi itakapotajwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles