Jennifer Lopez avishwa pete ya uchumba

0
947

NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya kuwa kwenye uhusiano kwa miaka miwili, hatimaye nyota wa muziki nchini Marekani, Jennifer Lopez ‘J. Lo’, amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, Alex Rodriguez.

Wiki moja iliyopita, wawili hao walisherehekea kutimiza miaka miwili ya uhusiano wao, lakini mwishoni mwa wiki iliyopita Rodriguez aliamua kumvisha pete mrembo huyo mwenye umri wa miaka 49.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa nyota huyo wa zamani wa mchezo wa Baseball, alidai amefurahi kuona anakubaliwa kumvisha pete mrembo huyo.

Rodriguez (43) aliposti picha ya mkono wa J. Lo huku akiwa anamvisha pete na kuandika: “Amekubali.” 

Hii si mara ya kwanza kwa J. Lo kuvishwa pete ya uchumba, amewahi kufanyiwa hivyo mara sita na wanaume tofauti na aliwahi kufunga ndoa mara tatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here