24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Nicki Minaj awaomba radhi mashabiki Ufaransa

PARIS, UFARANSA 

STAA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Nicki Minaj, amewaomba radhi mashabiki nchini Ufaransa baada ya kusitisha kwa shoo yake kwa mara ya pili, ikiwa ni saa chache kabla ya kuanza kwa tamasha.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 36, aliweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo ilikuwa inaelezea sababu za kusitisha tamasha hilo.

“Hellow mashabiki zangu, sipendi kitendo cha kusitisha ziara yangu ya muziki wala kupoteza fedha na kuwafanya mashabiki zangu wakose furaha, napenda kufanya shoo mbele ya mashabiki zangu.

“Tatizo lililopo liko nje ya uwezo wetu, hivyo mambo yikikaa sawa kila kitu kitakuwa wazi, kwa sasa ukweli ni kwamba tupo nje ya uwezo wetu, lakini nawapenda sana mashabiki na sitaki kuwaangusha,” alisema mrembo huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,476FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles