22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Firmino, Mane waibeba Liverpool nyumbani

LIVERPOOL, ENGLAND 

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Roberto Firmino, jana aliibeba timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Burnley, akifunga mabao mawili katika ushindi wa 4-2 kwenye uwanja wa nyumbani wa Anfield.

Michuano hiyo ya Ligi Kuu England iliendelea jana kwa michezo mitatu kupigwa kwenye viwanja tofauti, lakini mchezo wa Liverpool ulikuwa wa kwanza na klabu hiyo kuibuka na ushindi huo.

Mbali na Burnley kuanza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la mapema, lakini wenyeji Liverpool waliweza kujipanga na kutafuta bao la kusawazisha na kuongeza mabao mengine.

Burnley walifanikiwa kupata bao katika dakika ya sita kupitia kwa kiungo wake, Ashley Westwood, baada ya kufanya shambulizi la mpira wa kona na kumfanya mchezaji huyo kuwa bao lake la kwanza kwa klabu hiyo kwa mkopo akitokea Aston Villa mwaka 2017.

Mshambuliaji wa Liverpool raia wa nchini Brazil, Firmino, hakutumia dakika nyingi kuonesha ubora wake wa kupachika mabao, dakika ya 19 aliweza kutikisa nyavu na kuisawazishia timu hiyo.

Dakika 10 baada ya bao hilo, Liverpool waliwainua mashabiki wake baada ya kuongeza bao la pili lililowekwa wavuni na mshambuliaji wao, Sadio Mane, baada ya shambulizi lililoanzishwa na Mohamed Salah.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Liverpool walikwenda mapumzikoni huku wakiwa mbele kwa mabao 2-1, lakini baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, bado walionekana kuwa na kasi huku wakitafuta mabao zaidi.

Firmino alionekana kuwa na kiu ya mabao, dakika ya 68 alirudi tena nyavuni na kuiandikia Liverpool bao la tatu, lakini wapinzani wao hawakukata tamaa mapema, walizidi kuonesha juhudi za kuongeza bao.

Dakika ya 90, Burnley waliweza kuongeza bao la pili kupitia kwa kiungo wake, Jóhann Berg Guomundsson, baada ya kazi safi iliyofanywa na Matej Vydra.

Zikiwa zimesalia sekunde chache mchezo huo kumalizika, Mane aliwainua tena mashabiki wa Liverpool baada ya kupachika bao la nne kwa timu hiyo, huku likiwa bao la pili kwake katika mchezo huo, hivyo hadi dakika 90 zinamalizika, Liverpool waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 4-2, huku wakiwa wanazidi kuwafukuzia wapinzani wao Manchester City ambao wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi moja dhidi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles