24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

JELA MIAKA 30 KWA  KUPORA PIKIPIKI 

Na ABDALLAH AMIRI


MAHAKAMA ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imewahukumu vijana wawili kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja kwa   wizi wa kutumia silaha.

Waliyohukumiwa na mahakama hapo ni Michael Machiya (25) mkazi wa kitongoji cha Itagata Kijiji cha Migandu mkoani Singida na Sanyiwa Mbalu (25) kutoka Kijiji cha Mgoroka Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi.

Awali Mwendesha Mashtaka wa Polisi WIlaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya, Ajali Milanzi kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Februari 6 mwaka huu   usiku katika  a mtaa wa Mwayunge barabara ya Mwanzugi Igunga mjini.

Washtakiwa wote wawili kwa pamoja walikuwa wakituhumiwa kuiba pikipiki   ya SANLG   yenye thamani ya Sh milioni 2.2 mali ya Mazinge Jumanne ambaye ni dereva wa bodaboda mkazi wa mtaa wa Mwayunge ambaye walimkata na kitu chenye ncha kali shingoni.

 Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo lakini mashahidi  watano  akiwamo muathirika wa tukio hilo   waliwatambua washtakiwa.

Kabla ya kutoa hukumu, Hakimu Ajali Milanzi alisema  mahakama imewaona wana hatia hivyo  alihukumiwa kwenda jela miaka 30 kila mmoja huku pikipiki  ikikabidhiwa kwa mwenye mali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles