27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SHEIKH   ATAKA WAZAZI WAFUNDISHE MAADILI

Na CLARA MATIMO


Mwenyekiti wa Jumuiya  ya kuendeleza Quran na Sunna Tanzania (JUQUSUTA), Sheikh Hasani Kabeke  amewataka wazazi na walezi kuwafundisha watoto wao uzalendo  watambua  thamani na utu wa binadamu.

 Amesema ili kurejesha maadili mema kwa jamii ni lazima watoto wakafundishwa uzalendo kuanzia nyumbani kwao.

Sheikh huyo aliwataka wazazi au walezi kuhakikisha watoto wao wanajua thamani ya ubinadamu na utu ikiwa ni pamoja na kulinda uhai.

Alisema hivi sasa kuna baadhi ya Watanzania kutoka dini zote ambao maadili yao siyo mazuri .

Kwa mujibu wa Sheikh Kabeke,  hali hiyo inaanzia katika ngazi ya familia ndiyo maana kuna familia nyingine ambazo wakubwa na wadogo wote hawajui nafasi yao.

“Maadili yamemomonyoka kuanzia  ngazi ya familia, leo mtu anajiona yeye anaweza kufanya kila kitu   tofauti  na zamani.

“Enzi za wazee wetu wao waliamini maisha ya pamoja, kuheshimiana hata na watoto wa jirani na mtu mzima yoyote bila kujali kuwa ni mzazi wako aliweza kumkemea mtoto wa jirani lakini siku hizi hakuna jambo kama hilo.

Alisema hata lugha ambazo baadhi ya wasomi wanazotumia ikiwa nipamoja na mavazi wanayovaa vyuoni ni za kustaajabisha, haziendani na elimu waliyonayo hivyo kusababisha kupotea kwa uadilifu.

“Leo kila mtu fikra yake anataka awe tajiri…hakuna anayekataa utajiri lakini ni vizuri upate maisha mazuri katika hali ambayo Mungu ameiridhia.  

“Wito wangu ni kwamba wale wanaojitambua waendelee kujitambua vizuri na kumtii Mungu wao bila kujali dini, kabila itikadi za vyama wala ukanda.

“Jambo muhimu ni kuweka utanzania wetu mbele maana mimi huwa naamini matendo   mazuri yanakubalika katika dini zote.

Aliwataka watumishi wa Mungu waendelee kutenda mambo mazuri ambayo Mungu anayaridhia na wanajamii wote kupitia dini zao na imani zao watende yale ambayo jamii inayaridhia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles