23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Hofu yaghubika Mkutano Mkuu TFF

NA OSCAR ASSENGA

VIONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA), wameingiwa na hofu kuhusiana na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), uliopangwa kufanyika katika Hoteli ya Regal Naivera, baada ya kushindwa kuelezea maandalizi yake.

Akizungumza mkoani hapa, Msimamizi wa Kituo cha Tanga na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF Mkoa wa Tanga, Khalid Abdallah, alisema wao hawawezi kuzungumzia maandalizi ya mkutano huo kwa sababu maelezo yanatolewa na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto.

“Unajua huo mkutano ni wa TFF na kama unavyojua TFF ina taratibu zake na kanuni, hivyo suala hilo anaweza kulizungumza mhusika ambaye ni Ofisa Habari wa shirikisho hilo,” alisema Abdallah.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Hoteli ya Regail Naivera mahali ambako kutafanyika mkutano huo, Primus Msele, alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na wanaendelea na matayarisho.

“Niseme maandalizi kwa upande wetu yamekamilika asilimia kubwa na sasa naweza kusema yapo vizuri na ulinzi utakuwepo wakati wote wa mkutano huo,” alisema.

 Mkutano huo wa TFF, unafanyika kwa mara ya kwanza tangu ulipoingia madarakani uongozi wa Rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi.

Hofu ya kutofanyika kwa mkutano huo inatokana na ukosefu wa fedha baada ya wiki iliyopita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Ilala kuzuia fedha kwenye akaunti zote za TFF kwa madai ya kulipwa kiasi cha shilingi 1,637,334,000 (bilioni 1.6) ikiwa ni kodi kwa kipindi cha 2010-2013 ambayo sehemu kubwa ikiwa ni makato ya kwenye mishahara ya walimu wa kigeni, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Jacob Michelsen na vile vile kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Brazil uliofanyika 2010.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles