26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ni mtihani wa Kerr kwa Azam

simba-vs-azamMSHAMU NGOJWIKE

KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, leo atakuwa na mtihani mgumu wakati timu yake itakapokabiliana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Kerr mwenyewe ameingiwa na wasiwasi ambapo amesema Azam FC ni timu nzuri, lakini atahakikisha timu yake inapata ushindi kwenye mchezo huo.

Simba imerejea juzi ikitokea Zanzibar ilipoweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na ligi hiyo na jana ilifanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo Kerr alitoa maelekezo kuhakikisha anapata ushindi katika mchezo huo.

Akizungumza katika mazoezi hayo, Kerr alisema anaiheshimu Azam kwa kuwa ni timu nzuri kwa sasa Tanzania lakini hawawezi kufungwa katika mchezo huo.

“Azam ni timu nzuri, wana wachezaji wengi wa kimataifa wenye uwezo wa hali ya juu, lakini sisi tunahitaji ushindi zaidi ya wao sasa lazima tushinde.

“Mchezo huu ni mgumu kutokana na Azam wanasaka matokeo na sisi tunataka matokeo zaidi yao, tutahakikisha tunashinda ili tujisogeze juu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema.

Kuelekea katika mchezo huo, Kerr aliwachambua wachezaji wake ambao atawapa nafasi ya kucheza leo ambao kwake anaona utakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu wanayokutana nayo.

Alisema kwa makipa waliokuwepo kati ya Vincent Angban na Peter Manyika, wote ni bora lakini Angban ana uzoefu wa hali ya juu moja kwa moja atakuwa kipa namba moja.

Alimtaja Hassani Ramadhani ‘Kessy’, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassani Isihaka, Jjuuko Murshid na Justice Majabvi, ndio wataunda ukuta wa klabu hiyo katika mechi hiyo.

“Nina mabeki wengi kila mmoja ana uwezo wa hali ya juu, lakini kama Mohamed Fakhi amekaa nje kwa miezi sita, sasa hawezi kuingia kikosi cha kwanza,” alisema.

Alisema katika safu yake kiungo na ushambuliaji atawapanga Ibrahim Ajib, Said Ndemla, Hamis Kiiza, Paul Kiongera na Brian Majwega.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles