24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Majeruhi waitesa Yanga

755252_heroaNA OSCAR ASSENGA

 

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo itakuwa ugenini katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kukabiliana na wenyeji, Mgambo Shooting huku ikiwa na wachezaji majeruhi wanaowategemea.

 

Wachezaji ambao huenda wakakosekana katika mechi hiyo ni Donald Ngoma na Haruna Niyonzima.

 

Akizungumza jana mjini hapa, Meneja wa timu hiyo, Hafidhi Salehe, alisema kuwa Ngoma atashindwa kucheza mechi hiyo kutokana na kusumbuliwa na majeruhi aliyopata hivi karibuni wakati wa mechi waliyokuwa wakicheza Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya Ligi Kuu.

 

Alisema kutokana na kusumbuliwa na tatizo hilo alishindwa kufanya mazoezi juzi katika Uwanja wa Mkwakwani huku wachezaji wenzake wakishiriki mazoezi hayo yaliyokuwa yakiendeshwa na Kocha Mkuu, Hans Pluijm.

 

“Hawa wachezaji watashindwa kucheza kwenye mechi ya kesho (leo) lakini hilo halitupi tabu, tumejipanga vizuri kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwa sababu hiyo ndiyo dhamira yetu kubwa iliyotuleta Tanga,” alisema.

 

Hata hivyo, alisema licha ya kutokucheza wachezaji hao lakini wengine wataikosa mechi hiyo ambao ni Nadiri Haroub ‘Cannavaro’, Oscar Joshua na Salum Telela ambao wamebaki Dar es Salaam.

 

Akimzungumzia Haruna Niyonzima, Hafidhi alisema kuwa mchezaji huyo tangu amalize majukumu yake kwenye timu ya Taifa ambayo alikwenda kuichezea mpaka sasa bado hajajiunga na kikosi cha timu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles