29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mtibwa Sugar mwendo ni ule ule

mtibwa-picha-1NA ZAINAB IDDY

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, amesema licha ya kutofanya usajili katika kikosi chake hadi sasa katika usajili wa dirisha dogo, mwendo wao utakuwa ni ule ule kama walioanza nao Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Katika msimamo wa ligi hiyo hadi sasa Mtibwa Sugar imecheza mechi tisa ambapo imeshinda mechi saba, sare moja na kupoteza mmoja.

Kwa matokeo hayo, Mtibwa inashika nafasi ya tatu katika msimamo  wa ligi hiyo wakiwa na pointi 22 nyuma ya Yanga waliopo nafasi ya pili kwa pointi 23 na Azam  wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 25.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Mexime ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, alisema licha ya kutokuwepo na mabadiliko makubwa katika kikosi chake bado kitaendelea kutembeza dozi kwa kila timu watakayokutana nayo.

“Tulivyoanza ndivyo tutakavyomaliza kwani lengo letu ni kuona msimu huu Mtibwa inamaliza katika nafasi tatu za juu baada ya kushindwa kuyafikia malengo hayo kwenye kipindi kirefu kilichopita.

Mtibwa Sugar leo itakuwa ugenini katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya kuwakabili wenyeji wao, Mbeya City.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles