24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Gabon yafungia kituo cha runinga Cameroon

Libreville, Gabon



Mamlaka Kuu ya Mawasiliano nchini Gabon, HAC, imesimamisha kituo cha runinga cha Cameroon, kwa kutoa taarifa ya uongo juu ya kifo cha Rais Ali Bongo Ondimba.

Kituo hicho (The vision 4) mwishoni mwa wiki iliyopita kiliripoti kwamba Bongo, amefariki hospitali ya Saudi Arabia, akiwa mapokezi.

HAC, imesimamisha kituo hicho cha runinga kurusha matangazo nchini Gabon na sasa Warushaji wakuu wa matangazo ya runinga nchini humo ni Canal +, Sat-Con na TNT Africa.

Mamlaka ya udhibiti wa urushaji matangazo ya runinga nchini humo umesema kituo hicho cha Cameroon kimeathiri maisha ya wengine kwa kueneza taarifa inayojaribu kuharibu utaratibu wa kutoa taarifa kwa umma.

Kufuatia ripoti ya kifo, serikali ilifafanua katika taarifa rasmi kwamba Rais huyo alikuwa na matatizo kutokana na uchovu na ratiba yake ya kazi ya ndani na kimataifa.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba Rais Ondimba anaendelea vizuri na yupo katika hospitali ya King Faisal, chini ya uangalizi wa madaktari na matibau zaidi.

Siku ya Jumapili, Ubalozi wa Kameruni, huko Gabon, ulitoa taarifa ambayo ilitangaza kuwa serikali ya Cameroon, imejitenga yenyewe kutoka kwenye taarifa iliyopatikana kwa kituo hicho cha matangazo (The vision 4).

Taarifa hiyo imesema kifo kilichoripotiwa na kituo hicho ilikuwa kinyume na mahusiano ya kikabila yaliyopo kati ya Rais wa Cameroon, Paul Biya na mwenzake wa Gabon, Ali Bongo Ondimba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles