23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Upinzani wahofia uchaguzi wa Desemba 23 DRC

 Kinshasa, DR Congo



Viongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wana wasiwasi juu ya uchaguzi wa Rais unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu.

Viongozi wanaouunda mshikamano wa Chama cha Uraia na Maendeleo wamesema misaada uliotolewa kwa jeshi wa malori zaidi ya 150 na ndege kadhaa katika kipindi cha uchaguzi wa nchi inachanganya.

Tume ya uchaguzi ya DR Kongo (CENI), imesema malori 300, ndege 10 na helikopta 10 zitatumika kusambaza vifaa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwenye uchaguzi mkuu wa Desemba 23.

“Mimi binafsi sina imani na mchakato huu, taarifa za jeshi kutoka kwa kwa kamanda mkuu, ambaye chama tawala kimemchagua mgombea wake, lakini sasa tuna jeshi, ambalo limetoa huduma zake kwa CENI lakini hatujui ikiwa ni CENI ambayo inadhibiti vifaa vya uchaguzi , kama malori au ndege zitakazosambaza nyenzo za uchaguzi zitaongozwa na madereva kutoka jeshi. Kwa hivyo serikali inataka kutufanya tuwe na wasiwasi na kufikiri kwamba tunashiriki katika uchaguzi au  hatushiriki,” amesema Alex Dende ambaye ni kiongozi wa upinzani.

Vyama vingine vya upinzani vinasema, hii ni ishara nyingine kwama nchi haitakuwa na uchaguzi huru na wa haki.

Serikali imekataa matangazo ya ushauri, uangalizi na ufadhili wa uchaguzi kutoka nje ya nchi.

Tayari, kumekuwa na maandamano dhidi ya matumizi ya teknolojia ya kupiga kura katika uchaguzi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles