25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Fukuta: Fedha za BSS naziingiza kwenye muziki

Beatrice Kaiza

MSHINDI wa shindano la kusaka vipaji, Bongo Star Search (BSS), mwaka 2019, Meshack Fukuta, amesema kuwa akipata fedha zake za ushindi ambazo ni milioni 20 atazitumia kwa ajili ya muziki wake na si kula bata kama watu ambavyo wanadhani.

alisema fedha hizo sio nyingi wala kidogo, lakini asipotuliza akili anaweza kuja kujikuta amezitumia bila ya kutimiza malengo yake.

“Sijapata fedha bado na ni lazima nijipange ili nisije kuchanganyikiwa, natarajia kupata mililioni 20 huku milioni 30 zikiingia moja kwa moja kwenye usimamizi wa kazi zangu, hivyo hata hizo milioni 20 nitaziingiza kwenye kazi ya muziki na sio kula bata,” alisema Meshack.

Aliongezea kuwa licha ya BSS kuwekeza Milioni 30 kupitia muziki wake kama mkataba wao unavyoeleza ila na yeye ameona ni bora kuwekeza fedha hizo kwa ajili ya muziki ili kutimiza malengo yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles