Kodak Black kutoka jela 2022

0
772

Miami, Marekani

KWA mujibu wa mtandao wa TMZ, rapa Kodak Black ataendelea kukaa jela kwa miaka miwili hadi Agosti 2022.

Kulikuwa na taarifa kwamba kuna uwezekano mkubwa wa msanii huyo kuwa huru mwishoni mwa mwaka huu, lakini mwishoni mwa wiki iliopita taarifa ya kumaliza kifungo chake iliwekwa wazi.

Hata hivyo kwa sasa amehamiswa gereza badala ya Miami na sasa amepelekwa mjini Oklahoma City, ambapo atakuwa huku hadi mwisho wa kifungo chake.

Msanii huyo alishtakiwa kwenda jela kwa miezi 46 kutokana na kukutwa na dawa za kulevya na silaha kinyume na sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here