24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

ENRIQUE: JUVENTUS WALITUWEZA MCHEZO WA KWANZA

BARCELONA, HISPANIA


BAADA ya Barcelona kukubali kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Juventus, kocha wa timu hiyo, Luis Enrique, amedai walifanya makosa katika mchezo wa kwanza nchini Italia.

Barcelona juzi walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani Camp Nou na kulazimishwa suluhu dhidi ya Juventus katika hatua ya robo fainali, hivyo kuifanya Juventus isonge mbele hatua ya nusu fainali kutokana na ushindi walioupata awali kwenye uwanja wa nyumbani wa mabao 3-0.

Kocha huyo wa Barcelona baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa juzi, alionekana kuwatupia lawama wachezaji wake kwa kushindwa kucheza katika ubora wao kwenye mchezo wa awali ambao ungeweza kuwasaidia kufanya vizuri katika mchezo uliofuata.

“Siwezi kuielezea Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa neno moja, lakini kikubwa ambacho naweza kusema ni kwamba Juventus wametuua kwenye mchezo wa kwanza wakiwa uwanja wa nyumbani. Nakumbuka kila kitu ambacho kilikuwa kinatokea kwenye mchezo huo hasa jinsi tulivyokuwa tunapoteza.

“Katika mchezo huo wa awali, Barcelona walishindwa kuonesha ubora wao na kupata bao la ugenini, hivyo waliwaruhusu wapinzani wao kupata mabao mengi yaliyowapa nguvu katika kulinda lango lao.

“Ninaamini kama tungeweza kupata bao ugenini, basi tungeweza kufanya vizuri, lakini kutokana na kushindwa kufanya hivyo mambo yakawa magumu kwenye uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki wetu. Lakini tumekutana na timu bora, yenye kocha bora,” alisema Enrique.

Hata hivyo, kocha huyo amedai nguvu zao kwa sasa wanazipeleka katika michuano ya Ligi Kuu nchini Hispania kwa ajili ya kutetea ubingwa, huku mchezo unaofuata ni dhidi ya wapinzani wao Real Madrid, Jumapili wiki hii.

“Mashabiki walitarajia makubwa kwenye Ligi ya Mabingwa, lakini kwa kuwa tumetolewa basi nguvu zetu zinarudi nchini Hispania kwenye Ligi Kuu ili kutetea ubingwa, tunaamini tunaweza kufanya hivyo,” aliongeza.

Timu nyingine ambayo juzi ilifanikiwa kuingia nusu fainali ni Monaco ambao walishinda mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao Borussia Dortmund, hivyo Monaco wanaungana na Real Madrid, Atletico Madrid na Juventus katika hatua ya nusu fainali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles