25.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

Ubunifu wa kiteknolojia unavyoibeba Exim Bank katika kuwahudumia wateja wake

Teknolojia imeendelea kuwa kitovu cha maendeleo ya jamii yetu kwa kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. Kukua kwa teknolojia katika nyanja mbalimbali za kiuchumi kisiasa na kijamii kumeendelea kuleta matokeo chanya siku hadi siku. Sambamba na kurahisishwa kwa utendaji kazi lakini pia upokeaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wa kawaida kumerahisishwa.

Katika kutambua fursa hiyo, kampuni mbalimbali za kiserikali na zile za binafsi hapa nchini zimeendelea kujidhatiti katika kuhakikisha kuwa zinatoa huduma kwa wananchi zinazoenda sambamba na mabadiliko hayo ya teknolojia.

Moja ya makampuni hayo ni Exim Bank. Kwa upande wake Exim imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inatoa huduma za kifedha kwa urahisi zaidi kwa wateja wake. Hayo yameelezwa na Meneja Bidhaa wa benki hiyo Ndugu Aloyse Maro ambaye amesema kuwa ubunifu wao kama Exim umekuwa ni chachu kubwa katika kurahisisha utoaji huduma kwa wateja wao.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=3G0xeFXUgtY[/embedyt]

Kupitia ubunifu wa kiteknolojia, Exim Bank imewezesha wateja kupata huduma mbalimbali kwa njia rahisi zaidi”. Maro ametaja huduma tatu ambazo ni matunda ya ubunifu wa kiteknolojia kuwa ni pamoja na huduma ya Mobile Banking inayomuwezesha mteja kutoa au kutuma pesa kwenye akaunti yake, kuangalia salio, kulipia bili ya maji au umeme na vingine vingi bila kupanga foleni.

Maro alieleza kuwa huduma ya pili ni ya ATM zinazopatikana nchi nzima zinazo muwezesha mteja kutoa pesa muda wowote. Huduma ya tatu ni kadi za kisasa zinazo muwezesha mteja kufanya malipo mbalimbali kwenye maduka makubwa na madogo pamoja na vituo vya mauzo vilivyoko ndani na nje ya nchi.

Moja ya faida kubwa itokanayo na teknolojia hii ni pamoja na kutunza muda. Mteja anaweza kufanya malipo yote na kupata taarifa za akaunti yake bila ya kutumia muda mrefu kwenda benki au kupanga foleni. Na hii ndio maana halisi ya kusema kuwa teknolojia inarahisisha maisha ya kila siku na kuboresha utendaji kazi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,173FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles