Cardi B ashtakiwa kwa kuwaumiza wasichana

0
910

NEW YORK, MAREKANI  

RAPA Belcalis Almánzar maarufu kwa jina la Cardi B, ameshtakiwa kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha wahudumu wawili wa ‘Night Club’ ambayo inajulikana kwa jina la Angels Strip Club, kuumizwa.

Polisi katika eneo la Queens, walimshikilia mwanadada huyo na kumfungulia mashtaka.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, mrembo huyo alianzisha vurugu kwa madai kwamba mmoja kati ya wahudumu aliwahi kuwa kwenye uhusiano na baba wa mtoto wake Offset.

Siku za hivi karibuni, mrembo huyo amekuwa kwenye mgogoro mzito na mkali wa muziki huo wa hip hop, Nicki Minaj na sasa jina lake linazidi kuwa kubwa kutokana na bifu hilo.

Matukio hayo yote anayafanya huku ikiwa ni miezi miwili tangu afanikiwe kupata mtoto wa kwanza, Kulture Kiari Cephus.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here