Mtewele awataka vijana kujiunga na vikundi wapate mikopo

0
1429

Raymond Minja, IringaMjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa anayewakilisha vijana, Theresia Mtewele, amewataka wajasiriamali wadogo kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa mikopo itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza wakati wa ufunguaji wa mafunzo ya ujasirilimali yaliyoratibiwa na Diwani wa Kata ya kitwitu, Baraka Kimatha na kutolewa na taasisi ya TAEDO Mtewele amesema wajasariliamali wengi wamekuwa hawakopesheki kwa sababu hawajajiunga katika vikundi.

“Ili kuendana na sera ya Serikali ya viwanda wajasiriliamali hawana budi kujiunga katika vikundi vidogo ili kupata mikopo itakayowasaidia kuanzisha viwanda vidogo jambo ambalo litawasaidia kuongeza kipato na ajira kwa watu wengine,” amesema.

Mtewele amesema ili mjasiriliamali aweze kufanikiwa lazima awe na nidhamu na fedha anayopata na si kuitumia hovyo kwani itasababisha kuyumba kwa biashara na hatimaye kufilisika.

Kwa upande wake Diwani Kimatha, amesema aliamua kutoa mafunzo hayo bure kwa wananchi wake ili kujikwamua kiuchumi na kujijengea ajira kuliko kusubiri kuajiriwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here