Kenyatta aguswa kifo cha mwanamuziki mkongwe Joseph Kamaru

0
1133

Nairobi, Kenya

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ameomboleza kifo cha mwanamuziki mkongwe nchini humo, Joseph Kamaru, akisema kifo chake ni pigo kwa sekta ya muziki wa Kenya.

Kamaru (79), amefariki kwenye Hospitali ya MP Shah, alikopelekwa kutibiwa Jumatatu wiki hii baada ya kuanguka.

Rais Kenyatta ametoa salamu zake za rambirambi kwa familia, jamaa, marafiki na mashabiki, akimuelezea mwanamuziki huyo maarufu kama mtaalamu mwenye ujuzi ambaye aliwahimiza na kukuza talanta za wanamuziki wengi wa Kenya.

Lakini pia alisema marehemu Kamaru, alitumia talanta yake kama mwanamuziki kushughulikia maadili wakati akiwa bora katika burudani.

“Ilikuwa baraka kwetu kama nchi kuwa na mtaalamu mwenye ujuzi ambaye alifanya jukumu kubwa katika kukuza muziki wa Kenya. Hakika tutakosa muziki wake wa elimu ambayo ilikuwa ya kipekee katika mambo mengi,” amesema Rais Kenyatta.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here