BET kumpa Mary J Blige tuzo ya heshima

0
457

LOS ANGELES, MAREKANI

MWANAMUZIKI mkongwe wa miondoko ya Pop na RnB, Mary J. Blige, anatarajia kutunukiwa tuzo ya heshima (Lifetime Achievement Award) kwenye tuzo za BET zitakazofanyika June 23-25, mwaka huu katika ukumbi wa Microsoft Theater, Los Angeles, Marekani  .

Mary J, ambaye aliwahi kuwa mshindi wa tuzo za Grammy mara tisa pamoja na kuuza album zake mara nane (multi-platinum) atatunukiwa heshima hiyo kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwenye tasnia ya muziki tangu mwaka 1992.


Imeelezwa kuwa, Mary J Blige ataungana na waimbaji kama Anita Baker wa mwaka jana, pia Charlie Wilson, Diana Ross, Whitney Houston, New Edition, James Brown na Prince wakiwa miongoni mwa mastaa waliopokea tuzo hiyo ya heshima.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here