26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

50 Cent amtuhumu wizi Bow Wow

NEW YORK, MAREKANI

MWEZI uliopita rapa 50 Cent, alikuwa anawataja hadharani wale ambao anawadai fedha ikiwa pamoja na rafiki zake wa karibu kutoka kundi la G-Unit, wiki hii pia staa huyo amemtaja rapa Bow Wow kuwa aliwahu kumwibia fedha.

50 Cent, ambaye alitamba na albamu yake ya Get Rich Or Die Try, alisema Bow Wow alikuja nyumbani kwake na wakapanga kwenda Night Club na yeye akatenga bunda za dola moja moja na kumpa msanii huyo kwa ajili ya kwenda kutupa kwa mashabiki wakiwa jukwaani.

Baada ya hapo, Cent alidai alishangaa kuona hadi wanaondoka kwenye ukumbi huo bila ya Bow Wow kutupa hata bunda moja la fedha, hivyo amemtaka kurudisha fedha hizo kwa kuwa ni sawa na wizi.

“Kitu ambacho alichokifanya Bow Wow siyo sawa, alichukua kiasi kikubwa cha fedha zangu kwa ajili ya kwenda kutupa kwa wachezaji wa muziki lakini hadi tunaondoka hakufanya hivyo, huo ni sawa na wizi, hivyo hadi kufikia Jumatatu nirudishiwe fedha zangu,” aliandika 50 Cent kwenye Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,631FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles