24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi wa Marekani atoa wito udumavu kumalizwa Kagera

RENATHA KIPAKA-BUKOBA

KAIMU Balozi wa Marekani nchini, Dk. Inmi Patterson, ametembelea miradi ya maendeleo mkoani hapa katika upande wa afya na kuutaka uongozi wa mkoa kufanya jitihada za kuondoa udumavu.

Akiwa mkoani hapa kwa ziara ya siku tatu, Dk. Patterson alisema lengo ni kufika katika miradi iliyofadhiliwa na Marekani kwani mkoa umekuwa ukifanya vizuri katika upimaji wa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) hasa kwa wanaume.

Hata hivyo Dk. Patterson alisema wananchi  wamehamasika kupima katika vituo vya afya na utumiaji wa dawa za kufubaza nguvu za virusi.

“Nimefurahi kufika hapa na kujionea miradi tunayoifadhili, kikubwa ni kuona maambukizi ya VVU na nashuja zaidi,” alisema Dk. Patterson.

Katika hatua nyingine, alisema licha ya kuwa na chakula cha kutosha, bado hali ya udumavu ni kubwa, lazima uongozi wa mkoa uchukue hatua kulingana na takwimu za sasa.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dk. Marco Mbata alisema  hatua mbalimbali zimechukuliwa na kufanikisha kupunguza asilimia zilikuwepo kutoka 41.7 hadi 39.8.

Alisema elimu iliyotolewa juu ya matumizi bora ya lishe yenye kutumia chakula aina mbalimbali kuondokana na mlo mmoja wa ndizi kutwa nzima ilizaa matunda.

Naye Mkuu wa Mkoa, Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema kwenye mkoa huo kuna fursa  mbalimbali za uwekezaji ikiwemo  kilimo, ufugaji na utalii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles