31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Magufuli ateua wajumbe bodi ya Airtel Tanzania

Mwandishi Wetu

Rais John Magufuli amemteua Mohammed Mtonga kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo Juni 12, akichukua nafasi ya Dkt. Omari Nundu ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania.

Uteuzi wa Dkt. Nundu umefuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya Bhart Airtel International juu ya uendeshaji wa kampuni ya simu za mkononi ambapo Mwenyekiti wa bodi hiyo anapaswa kuteuliwa na Tanzania.

Aidha kufuatia makubaliano hayo Afisa mkuu wa ufundi anapaswa pia kuteuliwa na serikali ya Tanzania ambapo aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo ni Dkt. Prosper Mafole.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles