22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kumshika sehemu za siri mtoto wa miaka mitatu

AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM

MKAZI wa Mbezi, Vicent Marseli (37), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam, akikabiliwa na shtaka la kumshika sehemu za siri mtoto wa miaka mitatu ili kujiridhisha kimapenzi.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Neema Moshi, alidai Februari 18 eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa alifanya shambulio la aibu kwa kumshika mtoto huyo sehemu za siri ili ajiridhishe kimapenzi.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na mwendesha mashtaka wa Jamhuri alisema upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Kiliwa alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya Sh 50,000 kila mmoja.

Hata hivyo, alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa Juni 25, mwaka huu.

Wakati huo huo, mahakamani hapo watu wawili wamepandisha kizimbani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Waliopandishwa kizimbani ni Stephano Shayo (22) na Abuu Kassim (22) Wakazi wa  Mbezi Bichi.

Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Neema Moshi, alidai Aprili 29 katika Barabara ya Bagamoyo eneo la Afrikana, Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa waliiba pochi moja ikiwa na simu ya Samsung H3 yenye thamani ya Sh 700,000, simu nyingine ya Samsung yenye thamani ya Sh 50,000 na fedha taslimu Sh 870,000 mali ya Sharifa Seleman. Kabla na baada ya kuiba walimtishia kwa kisu.

Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo, upande wa Jamhuri ulisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

HakimuKiliwa alisema shtaka hilo halina dhamana kisheria na kutaka washtakiwa kurudishwa rumande hadi Juni 25, mwaka huu shauri lao litakaposikilizwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles