24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Azam FC yamshukia Juma Nyosso

Juma-NyossoNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

TIMU ya Azam imepeleka barua rasmi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikiomba wamfungie beki wa Mbeya City, Juma Nyosso, kwa kitendo cha udhalilishaji dhidi ya nahodha wao, John Bocco.

Nyosso alifanya kosa hilo wakati timu yake ilipokubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Jumapili iliyopita, tukio lililokemewa vikali kwa watu mbalimbali wakitaka beki huyo aadhibiwe vikali.

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inatarajia kukutana muda wowote kuanzia sasa kupitia suala la beki huyo pamoja na mambo mengine.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Azam, Jaffary Idd, alisema uongozi wa timu hiyo umelaani vikali sana tukio la beki huyo, huku ukidai hawawezi kuingilia uhuru wa TFF katika kutoa adhabu stahiki kwa Nyosso.

“Tunawashukuru Watanzania wote, vyombo vya habari vilivyochukizwa na kitendo hicho na kuanza kukilaani. Lakini sisi kama Azam FC hatuwezi kuingilia uhuru wa TFF.

“TFF kupitia kamati yake ya nidhamu, ndio inaweza kukaa na kutoa uamuzi kwamba ni adhabu gani impe huyo mchezaji kutokana na sheria zilizopo zinazotokana na kosa lake,” alisema.

Azam imeomba itolewe adhabu inayoendana na Kanuni za Ligi za shirikisho hilo, 37(24) za udhibiti wa wachezaji inayoeleza kuwa: “Mchezaji yeyote atakayepatikana na hatia ya kufanya makosa makubwa ya kimaadili au kinidhamu, au ya kibaguzi, au ya kidhalilishaji, au yatakayotafsiriwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za mchezo na ubinadamu, atatozwa faini ya kati ya Sh milioni moja mpaka milioni tatu au/ kusimamishwa kushiriki michezo mitatu mpaka 10 ya klabu yake yoyote atakayoitumikia katika Ligi Kuu na mashindano mengine ya TFF au kufungiwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miwili.”

Hiyo ni mara ya pili ndani ya mwaka huu Nyosso kufanya tukio hilo, mara ya kwanza ilikuwa Machi, alipomdhalilisha aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Elias Maguli, katika mechi yao msimu uliopita na kupelekea kufungiwa mechi nane.

Wahanga wengine wa tukio hilo ni beki Amir Maftah, wakati akiichezea Yanga kwenye mchezo na Simba, ambapo baada ya kufanyiwa hivyo alimpiga kichwa na kutolewa kwa kadi nyekundu kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji Joseph Kaniki.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles