24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kibadeni: Simba itajuta kwa Tambwe

kibadeniNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

KOCHA mkongwe nchini na Mshauri wa Ufundi wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Abdallah Kibadeni ‘King’, amesema kuwa Simba itajutia sana kitendo cha kumuacha mshambuliaji, Amissi Tambwe na kusajiliwa na Yanga, akidai ni mmoja wa washambuliaji bora kwa sasa katika Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Kibadeni ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache mara baada ya Tambwe kung’ara kwenye mechi ya watani wa jadi, kwa kuifunga timu yake hiyo ya zamani kwenye ushindi wa Yanga wa mabao 2-0 Jumamosi iliyopita.

“Mimi nilisema na nitaendelea kusema kuwa Tambwe ni mshambuliaji mzuri wa kutupia mabao nyavuni, Simba ilikosea sana kumuacha. Tambwe hafanyi makosa akipata nafasi, hata ile mechi ya Yanga uliona alivyofunga,” alisema.

Tokea aachwe na Simba msimu uliopita, Tambwe alifunga mabao 13 akiwa Yanga na msimu huu mpaka sasa amefunga mabao manne na kutoa pasi za mabao manne, akimkaribia mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza, aliye kileleni kwa mabao matano.

Kocha huyo na mchezaji wa zamani wa Simba alisema Simba ilitawala sana mchezo huo, lakini kutokuwa na mshambuliaji bora namba 10 wa kusumbua ngome ya Yanga kulichangia wasipate matokeo ya ushindi.

“Simba ilitengeneza nafasi kadhaa, lakini hakukuwa na umakini, hata mabao tuliyofungwa yalitokana na uzembe wa mabeki kutowakaba vema washambuliaji wa Yanga,” alisema.

Hata hivyo, licha ya maandalizi ya makubwa waliyofanya timu zote visiwani Zanzibar kuelekea mechi hiyo, Kibadeni amedai haukuwa mchezo mzuri kama ilivyotarajiwa.

“Simba na Yanga kioo kwa timu nyingine, walifanya maandalizi makubwa, lakini ukubwa wa mchezo huo ulikuwa hauendani na kile kilichoonyeshwa na pande zote mbili,” alisema.

Kibadeni ndiye anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’, kwenye mchezo wa watani wa jadi Julai 19, 1977, kwenye ushindi wa Simba wa 6-0, rekodi ambayo haijavunjwa mpaka sasa.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles