30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

G Nako aeleza sababu za ‘Weusi’ kutokufa

3865247de9LNA SHARIFA MMASI

RAPA mahiri kutoka kundi la Weusi lenye maskani yake mkoani Arusha, George Mdemu ‘G Nako’, amesema
upendo, umoja, kutodharau na kufanyia kazi ushauri wa mashabiki wao ndiyo misingi inayoliwezesha kundi hilo lisivunjike kama makundi mengine yaliyowahi kuwika kwa muda mfupi kabla ya kusambaratika.

“Sababu hizo tuliziweka kwa pamoja wakati tulipoanzisha kundi letu hilo ambalo kwa sasa ni kampuni.
“Makundi mengi yanasahau kwamba nidhamu ni kitu muhimu katika kila kazi, wengi wao hujitazama binafsi husahau mafanikio ya kundi, huja kwa kuzingatia misingi hiyo tunayotumia sisi na kujikana mwenyewe kwamba ni zaidi ya wenzako,” alisema G Nako na kuongeza:
“Pia sisi tuna kitu kimoja tunakiita heshima kwa mdogo na mkubwa ndiyo maana hatukatai ushari wa yeyote hata ukiwa wa kutuponda tunafanyia kazi ili tukitoka awamu nyingine yule aliyetuponda awe mshabiki wetu, hatupunguzi
mashabiki bali tunaongeza,” anasema G Nako

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles