AY,MKEWE WAPATA MTOTO WA KIUME HUKO MAREKANI

0
606


Na Bethsheba Wambura,Dar es Salaam

IKIWA imepita miezi sita tangu mwanamuziki, Ambwene Yessayah (AY) na Remy wafunge ndoa usiku wa kuamkia Jumatatu Agost 13,2018 leo wamebarikiwa kupata mtoto wa kiume waliyempa jina la Aviel lenye maana kwamba ‘God is my father’,.

Akitumia ukurasa wake wa Instagram kuweka wazi kuhusu ujio wa mtoto huyo AY ameandika kwamba mkewe amejifungua katika hospitali ya Medical City Healthcare Dallas- Texas huko Marekani.

“Mungu ni mwema na namshukuru sana kwa kutubariki mimi na mke wangu mrembo Remy, tumempata mtoto wa kiume na tumempa jina la Aviel lenye maana ya ‘God is my father’, ameandika AY.

AY na Remy ambae ni raia wa Rwanda walifunga ndoa Februari 24,mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo kulihudhuriwa na mastaa kibao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here