24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

WAVAMIZI PORI LA KIGOSI KUONDOLEWA

 

Na Editha Karlo, Kigoma


SERIKALI  ya Mkoa wa Kigoma, inatarajia kuendesha operesheni ya kuwaondoa wafugaji waliopo katika Pori la akiba la Kigosi Muyowosi lililopo wilayani Kibondo ili kunusuru uhifadhi wa pori hilo pamoja na wanyama wanaopatikana humo.

Maamuzi haya yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Mstaafu Emmanuel Maganga, katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi wan a wadau ambapo pamoja na mambo mengine waliangalia namna ya kuendesha operesheni hiyo katika maeneo ya hifadhi.

“Kimsingi wafugaji waliopo pori la Muyowosi wanapaswa kuondoka haraka wasingoje tuwaondoe kwani taarifa zinaonesha tangu mwaka 2003 wafugaji hao walilipwa fidia na kutafutiwa eneo la kwenda hata hivyo wachache waliendelea kubaki.

“…na kuendelea kubaki kwako kwenye eneo hili la hifadhi ni kinyume na sheria, sisi tutaenda kuwaondoa, wale walioanza kuondoa nawapongeza kwa hatua hiyo ya kutii maagizo ya serikali,” alisema Brigedia Maganga.

Taarifa za serikali zimebaini kwamba kuna jumla ya wafugaji 44 ambao wanakadiriwa kuwa na mifugo zaidi ya 30,000 inayofungwa kwenye Pori la Akiba la Kigosi –Muyowosi.

Hata hivyo wamekuwa wakidai kuwa mazingira ya kuondoa mifugo yao ni magumu kutokana na eneo walilopo kuzungukwa na maji ya Mto Malagarasi, ajmabo linaloendelea kuathiri Ikolojia pamoja na wanyama pamoja na vitalu vya uwindaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles