24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI KAIRUKI AWAVUTIA PUMZI WACHIMBAJI RUBY

 

 

Na ELIYA MBONEA, ARUSHA


SERIKALI imeahidi kutoa uamuzi mgumu dhidi ya mgogoro wa mtobozano unaowakabili wawekezaji wa migodi ya madini ya vito ya Ruby, wilayani Longido, Mkoa wa Arusha.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Madini, Angela Kairuki, alipotembelea migodi ya kuchimba madini hayo ya vito ya Mundarara Ruby Mining na Sendeu Agrovet Investmet iliyopo Kata ya Mudarara.

Ruby inatajwa kuwa na thamani kubwa katika kundi la madini ya vito kwa kuwa Caret 1 inauzwa kati ya Dola za Marekani 6,000 hadi 7,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 13.6 hadi Sh milioni 15.8 za Tanzania.

Mtobozano huo unadaiwa kufanywa na Michael Laizer mbunge wa zamani wa Longido anayemiliki mgodi wa Sendeu na kuvuka mpaka wake na kuingia mgodi wa Mundarara Mining unaomilikiwa na mwekezaji, Rahimu Mollel.

Akizungumzia mgogoro huo baada ya kuitembelea migodi yote mwili na kujionea hali halisi, Waziri Kairuki aliwataka wawekezaji hao kutoa ushirikiano na kuacha kutunishiana misuli.

“Nimejionea, naamini mtafikia mwafaka. Natoa fursa ya mwisho, Jumatatu tatizo hili lianze kushughulikiwa na mkuu wa wilaya kwa kuwaita wote wanaovutana na pia wawepo maofisa wa madini ili kupata mwafaka wa pamoja haraka.

“Mkishindwa kuelewana, Serikali itaingilia kati na hapa mmoja atacheka au kulia au wote wawili kwani tutatoa uamuzi wetu mgumu kwa manufaa ya wananchi wa Longido.

“Kwa hiyo, nawaomba mkajipange kisaikolojia na pia angalieni namna gani mnaweza kuendelea na kazi kwa sababu sisi tunaangalia sheria kwa vile wataalamu wapo.

“Kama tutashindwa kutatua mgogoro huu, basi kutakuwa hakuna maana ya kuwapo wizara hii,” alisema Waziri Kairuki.

Kwa upande wake, Mollel ambaye ni Mmiliki wa Mgodi wa Mudarara, alisema mbali ya changamoto za mtobozano, atashiriki katika kukamilisha ahadi alizotoa kwa wananchi wa eneo hilo.

“Kwa ujumla, hadi sasa tunakwenda vizuri japokuwa mgodi ulioko jirani wametoboza na kuingia kwetu, lakini hatutaacha kurudisha kidogo tunachokipata kwa wananchi.

“Sisi kama mgodi, tutatoa tena Sh milioni 6 zilizobakia kwenye ujenzi wa nyumba ya walimu, kwani tayari mchanga na mawe upo na tulishatoa ahadi hii ambayo tutaikamilisha mapema,” alisema Mollel.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles