23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Rais arejea baada ya kuwakimbia nyoka ofisini

MONROVIA, LIBERIA

RAIS wa Liberia na nyota wa zamani wa soka George Weah, amerejea tena kazini wiki mbili baada ya kufurushwa na nyoka wawili waliokutwa katika jengo la ofisi yake.

Jengo hilo lilitakiwa kusafishwa vizuri kwa kemikali ya kuua nyoka kabla ya Rais huyo kushauriwa kurejea ofisini kwake juzi Jumatano.

Mmoja wa watu wa kwanza kumtembelea Weah katika ofisi yake alikuwa ni Makamu Rais wa zamani Joseph Boakai, aliyeshindwa na Weah katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017.

Weah alizungumzia juu ya juhudi za serikali yake za ‘kulinda misingi ya demokrasia na kuwavutia wawekezaji wa kigeni ili kuinua uchumi, taarifa hiyo ilitumwa kwenye tovuti ya Serikali.

Rais amekuwa akifanyia kazi katika ofisi iliyopo ghorofa ya sita ya jengo la Wizara ya Mambo ya Nje tangu jengo jirani na ofisi ya Rais lilipoungua kwa moto mwaka 2006.

Nyoka wawili weusi ambao walitoka kwenye shimo lilokuwa sehemu ya mapokezi ya jengo la ghorofa sita walikwenda nyuma ya jengo hilo ghafla wakati watu walipokuwa wakijaribu kuwaua.

Baada ya tukio hilo maafisa wa polisi na maafisa wa usalama wa rais walionekana wakiyalinda makao ya Weah katika mji mkuu wa Monrovia.

Kanda ya video iliyochapishwa katika ukurasa wa kwanza wa gazeti la African News ilionyesha wafanyakazi wakijaribu kuwashambulia nyoka wakati walipoonekana katika eneo la kukaribisha wageni la jengo hilo.

Jumba hilo limekuwa katika eneo hilo kwa miaka kadhaa sasa kwasababu ya mfumo wa maji taka, na maafisa wanasema kuna uwezekano wa nyoka kuingia katika jumba hilo.

Haijafahamika iwapo nyoka hao waliuawa au laa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles