23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani, Urusi zatunishiana misuli Venezuela

CARACAS, VENEZUELA

MZOZO wa kuwania madaraka nchini Venezuela kati ya Rais Nicolas Maduro na Spika wa Bunge, Juan Guaido, unazidi kufukuta, huku Urusi na  Marekani zikitunishiana misuli kuhusu taifa hilo la Amerika ya Kusini.

Juzi Jumatano Guaido aliitisha tena maandamano makubwa ya umma kwenye mitaa ya mji mkuu Caracas, lakini vyombo vya usalama viliyadhibiti huku wanajeshi wakigoma kuitikia wito wake wa kuungana na wenzao walioasi kumpindua Maduro.

Guaido alisema kungelifanyika kile alichokiita maandamano makubwa kabisa katika historia ya Venezuela na kuwa tayari mamilioni ya raia walikuwako mitaani.

Aliita hiyo awamu ya mwisho ya kumuondoa Maduro, lakini wengi wa waandamanaji waliondoka mitaani na kurejea majumbani mwao.

Rais Maduro kwa upande wake aliwahutubia wafuasi wake, akikanusha vikali kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo kuwa alikuwa tayari kuachia madaraka na kukimbilia Cuba kama si uingiliaji kati wa Urusi.

Maduro alisema viongozi wa Marekani ulikuwa unadanganywa na wapinzani wake ili kuwasaidia njama ya kumuondoa, lakini hilo lisingelifanikiwa.

“Jaribio lile la mapinduzi ambalo lilifanyika jana (juzi), upuuzi huo wa kupindua uliongozwa moja kwa moja kutoka Ikulu ya Marekani, na John Bolton.”

Mkwamo huu wa kisiasa unaongeza mzozo kati ya Marekani na Urusi, zinazotuhumiana kuingilia mambo ya ndani ya taifa hilo mwanachama wa Umoja wa Nchi Zinazozalisha Mafuta kwa wingi duniani (OPEC).

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo juzi alikiambia kituo cha Fox Business Network kuwa matumizi ya jeshi yanawezakana.

Lakini mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, alisema kuwa hatua yoyote zaidi ya uchokozi nchini Venezuela itakabiliwa na matokeo mabaya kabisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles