23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Zverev atwaa St Petersburg Open

alexander-zverevBERLIN, Ujerumani

NYOTA mwenye umri mdogo katika mchezo wa tenisi, Alexander Zverev, ameweza kutwaa ubingwa wa US Open kwa mara ya kwanza baada ya kumshinda mpinzani wake, Stan Wawrinka kwa seti 6-2 3-6 7-5.

Zverev mwenye umri wa miaka 19, ambaye anashika nafasi ya 27 kwa ubora duniani, ameweza kutamba mbele ya bingwa wa US Open anayeshika nafasi ya tatu kwa ubora kutoka nchini Switzerland, Stan Wawrinka.

Wawrinka, alionekana kupewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo na hasa kutokana na ubora wake katika viwango vya mchezo huo, lakini mashabiki ambao walijitokeza katika mchezo huo walionekana kuduwaa kutokana na kichapo alichokipata nyota huyo.

Wawrinka mwenye umri wa miaka 31, alianza vizuri katika seti ya pili na kuwapa nguvu mashabiki wake baada ya kupoteza seti ya kwanza, lakini alijikuta akiwa na kibarua kigumu katika seti ya mwisho na kupoteza mchezo huo.

“Ni jambo la kujivunia kwa upande wangu kwa kuwa nilikutana na mpinzani ambaye ana uwezo mkubwa katika tenisi, lakini nashukuru nimefanikiwa kutwaa ubingwa huo.

“Hii ni historia yangu mpya katika michuano mikubwa kama hii, ninaamini nitaweza kufanya makubwa zaidi kwenye michuano mingine kutokana na kile ambacho nimekifanya kwenye fainali hizi,” alisema Zverev.

Nyota mbalimbali wa mchezo huo wa tenisi wamempongeza Zverev kwa kutwaa ubingwa huo, hasa kutokana na umri wake kuwa mdogo na kushindana na mchezaji ambaye ana uzoefu mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,636FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles