30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 9, 2022

Drogba agombana na shabiki uwanjani

DROGBANEW YORK, Marekani

NYOTA wa klabu ya Montreal Impact, Didier Drogba, juzi aligombana na shabiki wa klabu ya New York Red Bulls, baada ya mchezo wao wa ligi kuu kumalizika.

Mshambuliaji huyo raia wa nchini Ivory Coast, alirushiana maneno na shabiki ambaye alikuwa karibu na mlango wa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, lakini walinzi wa uwanja huo waliweza kuwazuia wawili hao ambao tayari walianza kushikana mikono.

Drogba anadai kwamba baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kulikuwa na mashabiki wawili ambao walikuwa karibu sana na mlango wa kuingia kwenye vyumba ya kubadilishia nguo, hivyo aliwataka wasogee pembeni ili wachezaji wapite na ndipo vurugu hizo zikaanza.

“Kulikuwa na mashabiki wengi, lakini wawili kati ya hao walikuwa karibu sana na mlango na wala sikuwa na nia mbaya ila niliwaomba watupishe ndipo wakaanza kurusha maneno.

“Ni mambo ya kawaida kwa mashabiki kufanya mambo kama hayo, hasa pale timu yao inaposhinda au kufungwa,” alisema Drogba.

Katika mchezo huo, timu ya Drogba ilipoteza dhidi ya wapinzani wao, New York Red Bulls kwa bao 1-0, hivyo kuwafanya mashabiki wa New York kuwa na furaha kubwa uwanjani hapo.

Baadaye Drogba alitumia akaunti yake ya Twitter kuomba radhi kwa mashabiki ambao walijitokeza uwanjani hapo pamoja na wale walioliona tukio hilo kupitia mitandao ya kijamii.

Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya klabu yake ya zamani, Chelsea, kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Arsenal, hivyo mchezaji huyo alimpongeza mshambuliaji wa Arsenal, Theo Walcott, ambaye alifunga bao moja katika ushindi huo.

“Hongera sana kaka Theo Walcott kwa ushindi wenu dhidi ya Chelsea, lakini ninaamini ushindi huo ulikuwa mwepesi kwenu sawa na panya kucheza cheza kama paka hayupo katika eneo hilo,” alisema Drogba.

Drogba tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2015, amefanikiwa kucheza michezo 32 na kufunga mabao 21, huku akitoa pasi 6 za ushindi, akipiga mashuti 134, huku kati ya mashuti hayo, 55 yaliweza kulenga lango, ameoneshwa kadi ya njano mara 5 na kadi nyekundu mara 1.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,291FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles