24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Zoezi la Sensa laanza kwa mafanikio, waratibu wapewa neno

Na Hadia Khami,s Mtanzania Digital

Kamisaa wa Sensa Spika mstaafu, Anne Makinda amesema zoezi la sensa ya Watu na Makazi 2022 kwa siku ya kuamkia Agost 23, limefanikiwa kwa asimia 17.13.

Akizungumza na waandishi wa habariDar es Salaam Agosti 24, Makinda amesema kiwango hicho kimevuka malengo waliojiwekea kwa siku hiyo kwani walitegemea makarani watafikia asilimia 15.

Amesema zoezi litaendelea kwa muda wa siku saba hivyo ni vyema kwa wananchi kuwa na uvumilivu wa kwamba kila mwananchi ni lazima atahesabiwa.

“Yapo maneno mengi mtaani yanayosemwa kuhusu sensa na wakati mwengine inachanganywa sensa na uchaguzi ninachotaka kusema ni kwamba hii sensa ni siku saba lakini uchaguzi unafanyika siku moja,” amesema Makinda.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan kuitangaza Agost 23, kuwa Siku ya mapumziko ni kuiheshimisha nchi kwa sababu zoezi la sensa ni la umuhimu sanaa linafanyika kwa miaka 10 mara moja.

Aidha, amewataka waratibu wa sensa wa Wilaya na Mikoa kuweka namba maalum ambayo itatumika kwa ajili ya kueka ahadi kwa watu ambao hawaja hesabiwa.

Amesema kupiga cm hizo ni bure hazitakuwa na malipo lengo ni kutaja muda watakaokuwepo nyumbani kwao ili wafuatwe kwa lengo la kukamilisha zoezi.
Amesema vishkwambi vipo vya kutosha hata kama ikitokea vimepotea vipo vya ziada kwa ajili ya kukamilisha zoezi la sensa.

Hata hivyo amewataka viongozi wa serikali za mitaa kuwaongoza makarani wa sensa na kwa kila kiongozi mmoja anatakiwa amuongoze karani mmoja.

“Kwa kila kiongozi atalipwa kulingana na kumuongoza karani wala wasiwe na shaka kwani posho zao zipo,” amesema Makinda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles