30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

THRDC Zanzibar yaendesha mafunzo ya haki za binadamu kwa maofisa watekelezaji sheria


Na Asha Bani, Mtanzania Digital

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Zanzibar (THRDC-Zanzibar) unaendesha mafunzo kwa maafisa wa jeshi la polisi, maofisa kutoka ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) pamoja na maofisa kutoka Chuo cha Mafunzo (Magereza) Zanzibar.

Mafunzo ya siku mbili yameanza leo Augosti 24, katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel, Mjini Unguja huku mgeni rasmi akiwa ni Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar, Hamad Khamis Hamad.

Imeelezwa kuwa mafunzo hayo yamelenga kukuza uelewa wa masuala ya haki za binadamu na kuwakumbusha maofisa wa jeshi la polisi, mawakili kutoka katika ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali pamoja na maofisa wa chuo cha mafunzo (Magereza) kuendelea kufanya kazi kwa kufuata misingi ya haki za binadamu na kujadili changamoto zilizopo hususani za ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili wa watoto ili kushauriana namna bora ya kutatua na kuondokana na vhangamoto hizo.

Pia yameandaliwa kutokana na uwepo wa ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia visiwani Zanzibar ambapo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Juni, 2022 jumla ya kesi 487 za udhalilishaji ziliripotiwa, ukilinganisha na kesi 634 za udhalilishaji zilizoripotiwa kwa mwaka 2021, jambo linalopelekea jeshi la polisi pamoja na mamlaka mbali mbali kuhakikisha jitihada za ziada zinafanyika ili kumaliza kabisa changamoto hizo.

Mafunzo haya ni mwendelezo wa juhudi zinazofanywa na mtandao katika kuhakikisha wadau mbali mbali wa haki za binadamu hasa maofisa watekelezaji sheria wanafanya kazi kwa kufuata misingi ya haki za binadamu hasa katika utekelezaji wa majukumu yao pindi wanapohudumia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles