28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

ZIMAMOTO WATENGEWA MILIONI 100/-

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,  Thobias Andengenye

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

SERIKALI  imetenga Sh milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa ajili ya  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa itasaidia kupunguza upungufu wa sare za askari  wa jeshi hilo katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,  Thobias Andengenye alisema kwa mwaka huu mpya wa fedha, Serikali imeendelea kutatua changamoto za uhaba wa vitendea kazi ndani ya jeshi hilo.

Changamoto hizo ni kama vile magari na madawa ya kuzima moto ambako zimetengwa  Sh bilioni tatu mwaka huu wa fedha  kwa ajili ya kununua magari, ongezeko ambalo ni maradufu ya kiasi kilichotolewa mwaka wa fedha uliopita.

Alisema katika    mwaka wa fedha uliopita wa 2016/2017 Serikali ilitenga    Sh bilioni 1.5 kwa ajili ununuzi wa magari ya kuzima moto.

Alisema  jitihada hizo za Serikali  zinalenga kuondoa changamoto ya uhaba wa vitendea kazi na hivyo kurahisisha utendaji kazi wa jeshi hilo.

Kamishna Andengenye alisema mbali na ununuzi wa magari Serikali pia imeweka juhudi katika suala zima la ununuzi wa madawa ya kuzima moto ambako   Sh milioni 500 zimetengwa katika katika   mwaka huu wa fedha wa 2017/2018 kwa ajili ya ununuzi wa madawa ya kuzima moto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles