IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO POLISI

0
782
MKUU wa Jeshi la Polisi   (IGP) Simon Sirro
MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

MKUU wa Jeshi la Polisi   (IGP) Simon Sirro,  amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni   na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.

Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Jeshi hilo, Barnabus Mwakalukwa, ilieleza kwamba katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna  Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,  Suzan Kaganda,  amekuwa Mkuu wa kitengo cha Mafao na Fidia  Makao Makuu ya Polisi.

Nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Murilo Jumanne ambaye alikuwa kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga.

“Aidha nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Sylverius Haule, ambaye alikuwa Ofisa Mnadhimu  wa Polisi wa Mkoa wa Mara,” ilisema Mwakalukwa katika taarifa yake.

Alisema uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya  Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here