29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

ZIJUE SABABU 5 ZA UNITED KUSHINDWA KUTAMBA KATIKA USAJILI

 MOHAMED KASSARA

KLABU ya Manchester United imekuwa ikikumbana na ugumu katika harakati za kuboresha kikosi chao kwenye dirisha hili la usajili wa majira ya joto barani Ulaya kutokana na wachezaji wanaosaka kushindwa kuwapata. 

Mashabiki wa United wanashindwa kuelewa hali ya klabu hiyo kushindwa kunasa wachezaji hao licha ya ukubwa wan a utajiri wa timu hiyo. 

Wakati United ikihaha huku na huko, washindani wao Chelsea, Arsenal na Tottenham wameendelea kufanya kufuru kwenye soko la usajili kwa kushusha vifaa vya maana. 

Arsenal imesajili wachezaji sita katika dirisha hili kwa bajeti ya Euro milioni 40, wakiimarisha idara ya ulinzi na ushambuliaji. 

Tottenham imeizidi kete United katika mbio za kusajili wachezaji wawili kutoka Real Madrid ambao ni Gareth Bale na Sergio Reguilon ambao awali walitolewa macho na timu hiyo. 

Liverpool wako katika hatua za mwisho za kuwajili Thiago Alcantara, Ismailia Sarr na Diogo Jota, huku mahasimu wao, Manchester City wakiwanasa Ferran Torres na Nathan Ake. 

Chelsea ndo haishikiki kwenye dirisha hili baada ya kusajili wachezaji kadhaa wakiwemo Thiago Silva, Timo Werner, Kai Havert na Ben Chilwell. 

Wiki mbili sasa zimebaki kabla ya dirisha hilo kufungwa Oktoba 5, ambapo hadi sasa United imefanikiwa mchezaji mmoja tu ambaye ni kiungo Donny van der Beek kutoka Ajax. 

United ilikuwa katika mchakato wa kumsajili Jadon Sancho kutoka Dortmund, lakini dili hilo linaonekana kukwama baada ya kushindwa kulipa ada ya uhamisho inayotakiwa . 

Lakini hizi ni sababu tano za United 

 kushindwa kutamba katika dirisha hili la usajili 

KUSAKA WACHEZAJI WASIO SAHIHI 

United daima imekuwa na mazoea ya kuwafukuza wachezaji ambao hawawezi kupatikana. Mashetani hao Wekundu wametumia nusu muongo kuwafuata Gareth Bale, Antoine Griezmann, Thomas Muller, Cesc Fabregas na zaidi, ambao ni ghali sana, au hawana hamu ya kuondoka kwenye klabu zao. 

Hata katika dirisha hili United imejingiza katika mbio za kuwania mchezaji mwingine wa aina hiyo ambaye ni Jadon Sancho. 

Japokuwa Sancho ameweka wazi juu ya kutamani kurudi Ligi Kuu au klabu ya juu daraja la juu barani Ulaya, ada yake ya uhamisho inamfanya ashindwe kutua Old Traford kutokana na kushindwa kumudu gharama kutokana na hali yao ya kifedha. 

United inaonekana kupoteza muda wao mwingi wa kwa kumfuata Sancho, ambaye Dortmund hataki kumuachia, isipokuwa bei yao ya Pauni milioni 108 itafikiwa. 

Klabu hiyo sasa imeanza kufikiria njia mbadala baada ya kuona wazi kuwa hatawaweza kutoa kiasi hicho cha fedha kumnunua nyota huyo mwenye umri wa maiak 20. 

KUOGOPA KURUDIA MAKOSA 

Baada ya kufanya makosa ya mara kwa mara kwenye madirisha ya uhamisho, klabu hiyo inaishi kwa hofu au hufanya makosa sawa. 

Hapo zamani United walisaini wachezaji wenye majina kubwa kwa pesa nyingi, kama Alexis Sanchez, Angel Di Maria, Radamel Falcao, na Romelu Lukaku, ambao walilipwa pia mishahara mikubwa, lakini viwango vyao havikuridhisha. 

Wengi kati hao hawakufanikiwa na United ilipata hasara kubwa wakati wa kuuza wachezaji hao. Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward, anaogopa kufanya usajili mwingine kama huo, ambao utaleta hasara kubwa kwa klabu. 

Hii inaweza kuwa sababu ya United kuzidiwa kete na Tottenham katika mbio za kumsajili Gareth Bale. 

United ilihusishwa sana na uhamisho wa Bale, lakini labda walijitoa kwa sababu waliogopa mkataba kwa Bale ungefanana sana na ule wa Sanchez, ambapo walilazimika kulipa mshahara mkubwa kwa mchezaji ambaye alionesha uwezo mkubwa katika siku za nyuma. 

KUTOKUWA NA UWEZO KUONGEZA 

PESA ZA MAUZO 

Ole Gunnar 

 United kwa sasa ina wachezaji wengi kikosi chao ambao labda hawataki kuachilia au hawajapata timu. 

Wachezaji kama Jesse Lingard, Andreas Pereira, Phil Jones, Diogo Dalot, Marcos Rojo, na Chris Smalling wote wanaonekana hawana nafasi yoyote ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza. 

Smalling alitumia msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya AS Roma, ambapo alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kutumaniwa katika kikosi hicho. 

Lingard alihusishwa na kuhamia Everton au West Ham, angeweza kuuzwa na kuipatia klabu hiyo Pauni Milioni 20-30. 

Beki wa kulia Dalot pia amehusishwa na kuondoka, na inasemekana anapatikana kwa Pauni milioni 15, United ingeweza kutumia pesa hizo kuimarisha kikosi chao kwa kufanya usajili mpya. 

United italazimika kuwapiga bei mastaa wengine wa timu kama Marcos Rojo, Phil Jones na Andrea Pereira na uuzwaji wao ungeisadia timu kupunguza bajeti ya mishahara. 

KUKOSA CHAGUO MBADALA 

Hili ni tatizo ambalo tumeliona kwa United tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson. United, hutumia sehemu kubwa ya madirisha yao ya uhamisho, wakifuatilia mchezaji mmoja. 

United hapo zamani walipoteza kabisa muda katika uhamisho wakifuatilia Gareth Bale, Thomas Muller, Cesc Fabregas, Antoine Girezmann badala ya kubadili mawazo yao kwa chaguzi mbadala. 

Klabu hiyo imeonekana kupoteza muda mwingi wa dirisha hili la usajili ikimfukuza Sancho, badala ya kuzingatia chaguzi mbadala kama, Ousmane Dembele, Ismaila Sarr au Douglas Costa. 

United sasa italazimika kutumia wiki ya mwisho, au makubaliano ya siku ya mwisho, ambapo watalazimika kulipa fedha kubwa kwa sababu klabu zitatambua watalazimika kutoa ili kuboresha kikosi chao. 

KUKOSA ARI 

Hii inaweza kuwa sababu nyingine ya United kushindwa kutawala sokoni kama walivyokuwa zamani walijaribu kusajili wachezaji wakubwa na makocha wakubwa katika mchezo huo kuinua kuirudisha klabu hiyo kwenye viwango ilivyokuwa wakati wa Sir Alex Ferguson. 

United wameridhika na kikosi chao kwa sababu walipata nafasi ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita. 

Biashara ya uhamisho ya United inashindwa kuonyesha dalili zozote za klabu hiyo kujaribu kupunguza utofauti kati yao na Liverpool au Manchester City. 

Dirisha la uhamisho la United halikuwa la klabu ambayo inakusudia kupigania ubingwa wa Ligi Kuu au kwa bidhaa za fedha. 

Shughuli nyingi za uhamisho wa United inaweza kuwa chini ya ukosefu wa fedha kwa sababu ya janga la Corona au kwa sababu ya sera mpya ya uhamisho ya klabu hiyo . 

Mashabiki wa United wana wasiwasi juu ya mwelekeo gani klabu hiyo inaelekea na ikiwa msimu wa 2020-21 unaweza kupiga hatua mbili kurudi nyuma kuliko msimu uliopita. 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles