25.1 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Hamisa Mobetto apewa tuzo ya ubalozi bora Prima Afro

Jeremia Ernest

Mwanamitindo anayefanya vizuri ambae pia ni muigizaji wa filamu na msanii muziki nchini, Hamisa Mobetto amepewa tuzo ya ubalozi bora wa Kampuni ya nywele ya (Prima Afro) na kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 21, Hamisa amesema kuwa hakutarajia kupata tuzo hiyo ambapo ameshukuru kwa heshima hiyo aliyopewa.

“Sikutegemea kupata tuzo niliyoipata ni heshima kwa kuwa balozi bora na nimeongezewa mkataba wa mwaka mmoja ni nadra sana kwa wasanii mkataba unapoisha kuongezewa tena,” amesema Hamisa.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Prima Afro, Novatus Hekima, amesema kuwa wamemuongezea mkataba na kumpa tuzo kwa kufanyakazi kwake kazi kwa bidii kupitia ubalozi aliokuwa nao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles