27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

KOLABO YA ALICIA KEYS, DIAMOND YAUGUSA UBALOZI WA MAREKANI

 CHRISTOPHER MSEKENA 

WIMBO Wasted Energy ambao staa wa Marekani, Alicia Keys, amemshirikisha Diamond Platnumz, umeendelea kufanya vizuri kiasi cha kuugusa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania. 

Mapema jana Ubalozi wa Marekani ulitumia ukurasa wake wa Twitter kutoa ujumbe wa kufurahishwa na kolabo hiyo kwa kusema: “Inafurahisha kuona msanii wa Marekani Alicia Keys akimshirikisha msanii wa Kitanzania Diamond Platnumz, goma jipya la Wasted Energy ni moto.” 

Aidha, Alicia Keys ameshangazwa na mapokezi makubwa ya wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube ambapo umesikilizwa mara nyingi zaidi kuliko ngoma yoyote kwenye albamu yake, ALICIA. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles