23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

ZIJUE FAIDA ZA KUSOMA NJE YA NCHI

ASILIMIA kubwa ya Watanzania hupenda kwenda kusoma nje ya nchi jambo ambalo linaonekana kuwa ni la kawaida sasa.

Hulka hii inatokana na ukweli kwamba fursa za kusoma katika nchi nyingine zinaweza kumfaidisha mwanafunzi pindi atakapofika katika nchi husika.

Wanafunzi wanafursa ya kusoma katika nchi ya kigeni na kuona utamaduni na desturi za mazingira tofauti uliyoyazoea maishani mwao.

Sababu muhimu ambazo zinaweza zikakufanya kwenda kusoma nje:

 

Kuiona dunia

Sababu kubwa unapaswa kufikiria kusoma nje ni fursa ya kuona dunia kwa maana kuwa ndani ya sayari ya dunia zipo nchi nyingi hivyo nafasi ya kusafiri kutoka nchi moja hadi nyingine ni fursa muhimu kwa binadamu yeyote kujifunza mapya tofauti na nchi aliyotoka.

Hii itamsaidia pia kuchangamana na watu wenye mitazamo na desturi mpya.

Lakini pia mbali ya kufaidi mazingira ya nchi unayojipatia elimu pia upo uwezekano wa kusafiri au kutembelea maeneo mengine wakati wa masomo yako, unaweza pia kutembelea nchi za jirani.

Elimu

Sababu nyingine ni kupata uzoefu wa mambo mbalimbali na hata elimu tofauti.

Kwa kudahiliwa katika chuo cha nje, utakuwa na nafasi ya kuona upande wa pili wa taaluma yako ambayo usingeweza kuiona ukiwa katika nchi yako.

Utakuta mwenyewe umeanza kuzoea mfumo wa elimu wa nchi hiyo ikiwamo kuwaelewa watu, mila na utamaduni zao.

Elimu ni kiini cha masomo yako ukiwa nje kwa hiyo kuchagua chuo kizuri ni jambo la muhimu mno.

Fursa za kazi

Baada ya kumaliza masomo yako nje unarejea nyumbani na mtazamo mpya juu ya utamaduni, ujuzi wa lugha, elimu bora na nia ya kujifunza yote haya ni kuwavutia waajiri baadaye.

Maendeleo ya binafsi

Hakuna kitu kizuri kama kujitegemea katika nchi ya kigeni. Unaweza ukatambua kwamba kusoma nje hutoa fursa za kujitegemea.

Wanafunzi wanaosoma nje wanakuwa watafiti wa mambo mbalimbali katika nchi wanayosomea.

Manufaa ya kusoma nje ni nafasi ya kujitathimini mwenyewe wakati unaendelea kupata uelewa wa utamaduni tofauti.

Kuwa kwenye nchi ya kigeni nyakati zingine kunatosha kukujenga kimaisha lakini ni kipimo cha uwezo wako wa kukabiliana na hali ya maisha na wakati kuwa na uwezo wa kutatua matatizo.

 

Uzoefu wa maisha

Kwanini kusoma nje? Kwa wanafunzi wengi inaweza kuwa nafasi yao kupata kazi na fursa ya kusoma nje inaweza kugeuka kuwa ya mara moja tu katika maisha yako.

Kuchukua fursa hii kusafiri duniani kote kwa ajili ya kujifunza kuhusu tamaduni mpya. Kusoma nje ni uzoefu tofauti na kitu kingine chochote.

 

Kuhitimu

Kama waajiri baadaye, bodi ya wahitimu wa chuo kuangalia zaidi uzoefu uliyopata kama mwanafunzi kutoka nje.

Wanafunzi waliyosoma nje kuonyesha utofauti kwamba wao hawana hofu kukabilina na changamoto mpya au katika hali ngumu.

Cha muhimu zaidi, wanafunzi ambao walisoma nje waonyeshe ni kiasi gani walikuwa makini na elimu yao.

Vyuo vingi mara kwa mara kuangalia wanafunzi ambao wataleta mabadiliko ya kipeke katika chuo.

Pia wanatakiwa waonyeshe kwamba wao ni bora katika elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles