29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Zambia yashukuru kupewa hekta 20 na Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipa nchi hiyo hekta 20 za ardhi kwa ajili ya kuhudumia mizigo ya nchi hiyo.

Rais Hichilema amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari alioufanya na Rais Samia kwenye Ikulu ya Zambia iliyopo jijini Lusaka mapema leo Oktoba 25, 2023.

Rais Hichilema alisema Wazambia wamechukua hatua hiyo kama zawadi ya kuonyesha ushirikiano mwema baina ya nchi hizi mbili.

Katika hotuba yake kama mgeni rasmi wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia yaliyofanyika jana jijini Lusaka, Rais Samia alisema eneo ambalo Zambia itapewa liko Kwala, mkoani Pwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles