24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Zaidi ya wanaume 30,000 wafanyiwa tohara Simiyu

Derick Milton, Simiyu

Wanaume 33,950 katika mkoa wa Simiyu wamefanya tohara kinga katika kipindi cha muda wa miezi saba, kuanzia Oktoba 2018 hadi Aprili, 2019 ikiwa ni asilimia 57 ya lengo la kuwafikia wanaume 59,130.

Hayo yamesemwa leo Mei 8, na Mshauri wa huduma za tohara mkoa kutoka shirika la Intrahealth International, Dkt. Kentgen Evarist wakati akiongea na Mtanzania Digital ofisini kwake mjini Bariadi.

Dkt. Evarist amesema kuwa shirika hilo limejiwekea malengo ya kuwafikia wanaume 59,130 ambao bado hawajafanyiwa huduma hiyo, katika kipindi cha kuanzia Oktoba 2018 hadi Septemba 2019.

“Tumefanikiwa kuvuka nusu ya lengo letu ambalo tulijiwekea katika mkoa wa Simiyu, tuna imani hadi kufikia Septemba 2019 tutafanikiwa kuwafanyia tohara kinga wanaume wote ambao tuliwalenga,” amesema Dkt. Evarist.

Aidha amesema  shirika hilo kupitia mradi huo chini ya ufadhili wa mfuko wa Rais wa marekani wa kupambana na VVU (PEPFAR) kupitia CDC Tanzania, umepata mafanikio makubwa kwa wanaume wengi kujitokeza kufanyiwa tohara.

Shirika la IntraHealth International kwa kushirikiana na Kamati za Afya za Mikoa na Wilaya linatoa huduma ya Tohara kinga kwa wanaume katika mikoa ya Simiyu, Mwanza, Mara, Geita, Shinyanga, Kagera na Kigoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles