30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ummy Mwalimu: marufuku wanasiasa kuwaingilia madaktari, wauguzi

Arodia Peter, Dodoma

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepiga marufuku wanasiasa kuingilia fani za taaluma za madaktari, wakunga na wauguzi nchini.

Ummy ameyasema hayo bungeni leo, Mei 7 wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya wizara yake, ambapo amesema kama daktari, muuguzi au mkunga amekosea wapelekwe kwenye mabaraza yao ambayo ndiyo yanashughulikia suala la nidhamu kwa kada hiyo ya wstumishi.

“Kutokana na hali halisi ilivyo, muuguzi mmoja anafanya kazi ambayo ingefanywa na wauguzi watano na madaktari wanafanya kazi hivyo si vema kuwakatisha tamaa.

“Sisi kwa kutambua umuhimu wao tutaendelea kuwatetea wauguzi na madaktari wetu, tusiwakatishe tamaa na isitoshe hao wenye fedha hawaendi kutibiwa kwenye hizo hospitali za Serikali, matokeo yake wanaoumia ni watanzania,” amesema Waziri Ummy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles